Klabu ya jijini London, West Ham united imeshakamilisha usajili wa nyota wake wanne iliyowasajili katika kipindi hiki cha dirisha kubwa la usajili.
Alianza mlinzi wa kulia wa Manchester city, Pablo Zabaleta mwenye uraia wa Argentina kusajiliwa na klabu hiyo ambapo kwa mkongwe huyo wamemchukua bure mara baada wa kocha wa klabu hiyo ya Man city, Pep Guardiola kuamua kupigisha fagio kuachana na wachezaji wazee.
Akafata kipa pia wa Manchester city aliyetumia msimu uliopita kuichezea Torino kwa mkopo, Joe Hart ambaye kipa huyo wamemnasa kwa mkopo akionekana kutokuwa na nafasi ndani ya mipango ya Guardiola aliyemsajili kipa ghali kwa sasa, Ederson.
Nyota mwengine kumwaga wino klabuni hapo alikuwa Arnautovic aliyetokea Stoke city ambapo amefita hapo kwa kocha Slaven Bilic kufanya 'manuva'
Sasa jana nyota wa Mexico aliyekuwa anakipiga Bayer Leverkusen, Javier Hernandez 'Chicharito' alikamilisha usajili ndani ya klabu hiyo na kumfanya kuwa mchezaji anayepokea mshahara mkubwa kuliko mchezaji yoyote klabuni hapo. Anapokea paundi 140,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment