Kocha wa Chelsea, Antonio Conte huenda akaipiku kitita ambacho kimetumika na Pep Guardiola wa Manchester city katika kipindi hiki cha usajili.
Conte wa Chelsea mpaka sasa ameshatumia kiasi cha paundi milioni 132 kuwasajili nyota kama Antonio Rudiger, Tiemoue Bakayoko na Alvaro Morata wakati kwa upande wa Pep Guardiola ameshatumia kiasi cha paundi milioni 218.
Antonio Conte licha ya kuwasajili nyota hao lakini bado anatajwa kuwawania nyota wengine kama Alex Sandro wa Juventus anayetajwa kufikia thamani ya paundi milioni 60, Fernando Llorente na Antonio Candreva wote wanatajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 25 kila mmoja na mlinzi wa Southampton, Virgil van Dijk anayetwaja kuwa na thamani ya paundi milioni 60.
Kwa maana hiyo kama Chelsea itafanikiwa kuwanasa hao basi itakuwa imeipiku Manchester city katika kiasi cha pesa kilichotumika katika usajili.
No comments:
Post a Comment