Monday, 24 July 2017

China huenda ikaiazibu Chelsea

Nchi ya China ambayo inasifika kuwa nchi yenye sheria kali huenda safari hii ikaiangushia klabu ya Chelsea rungu la adhabu.

Hii huenda ikatokea mara baada ya siku kadhaa zilizopita ambapo Chelsea ilikuwa nchini humo ilipotakiwa kucheza mchezo wa kirafiki na Arsenal ndipo kijana Kennedy akatuma picha za mnato au video zilizoshutumiwa kuikashifu nchi hiyo.

Baada ya lawama nyingi ambapo raia na wapenda soka wa China kumshambulia mchezaji huyo raia wa Brazil ndipo mchezaji huyo akatuma ujumbe kupitia mtandao huohuo wa Instagram akiwaomba radhi raia wa nchi hiyo. Na baadae kidogo klabu nayo ikatuma ujumbe ikielezea jinsi safari yao nchini humo ilivyokuwa lakini pia ikiiomba China msamaha kwa kitendo kilichofanya na mchezaji wao.

Lakini kama inavyoeleweka, China ni kati ya nchi zenye sheria kali ikataarifiwa sekta au taasisi za kiserikali kutakiwa kufuta katika mitandao yao na mitandao yote ya habari kuhusu klabu hiyo ya Chelsea.

Kwa hatua hiyo ikatafsiriwa basi serikali ya nchi hiyo huenda ikaiadhibu klabu hiyo ya Chelsea.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.