Makinda na wachezaji wa Chelsea wazidi kutolewa kwa mkopo kwenda klabu nyengine. Achana na akina Ruben Loftus-cheek aliyetimkia Crystal Palace, au Kurt Zouma, Tammy Abraham au hata Kasey Palmer wengine hawa hapa.
Tomas Kalas naye amejiunga na Fulham kwa mkopo lakini kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya jijini London amesaini mkataba mpya na Chelsea utakaomweka hapo mpaka 2021.
Matt Miazga, mlinzi huyu aliyezaliwa mwaka 1995 mwenye uraia wa Marekani ameendelea kuwepo kwa mkopo barani Ulaya nchini Uholanzi alipokuwepo msimu uliopita akiitumikia Vitesse.
Jamal Blackman, huyu dogo naye ni kipa akiwa ametokea kwenye akademi ya Chelsea naye amejiunga na Sheffield United ambapo amesaini kuwepo Chelsea mpaka 2021.
No comments:
Post a Comment