Saturday, 29 July 2017

Conte na Pochettino pamechafuka

Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino amekasirishwa na maneno ya Antonio Conte ambaye ni kocha wa Chelsea juu ya mshambuliaji wake Harry Kane.

Antonio Conte alipoulizwa katika mkutano na waandishi wa habari juu ya mshambuliaji anayempenda akajibu "Ningemchagua Kane. Ni mshambuliaji aliyekamilika, nadhani ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani kwa sasa"

Antonio Conte ametoka kumsajili mshambuliaji mpya akitokea Real Madrid kwa dau la paundi milioni 70.

Lakini Pochettino ambaye ni mshindani wa Chelsea katika kuwania taji la ligi kuu msimu uliopita hajafurahishwa na maneno ya Conte na badala yake kasema "Nawaheshimu wachezaji wa timu pinzani, na naamini sio sahihi kufanya hivo"

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.