Saturday, 29 July 2017

Conte awalaumu akina Chalobah

Antonio Conte amechukizwa na jinsi makinda wa Chelsea wanavyoondoka klabuni hapo kwa kuuzwa wakijitetea wanataka nafasi.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameonekana kuuzunishwa na makinda wa klabu yake hiyo jinsi walivyoondoka kwa kuuzwa badala ya kutolewa kwa mkopo.

Nathaniel Chalobah aliyeuzwa kwenda Watford, Nathan Ake aliyeuzwa kwenda Bournemouth na Traore aliyeuzwa kwenda Olympique Lyon ndo kama wamemfanya kocha huyo muitaliano kuchukizwa.

"Tatizo la wachezaji wachanga au makinda wanashauriwa vibaya na wazazi na watu wao wa karibu wanapowaambia wanatakiwa kucheza kikosi cha kwanza, wanafikiri mpaka kucheza kikosi cha kwanza ni jambo rahisi sana" alisema Antonio Conte aliyeisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu Uingereza na kuifikisha klabu hiyo fainali ya kombe la FA.

Lakini pia siku kadhaa nyuma alihojiwa kuhusu ubora wa Bakayoko kumfanya Chalobah auuzwe ambapo baadhi ya wachambuzi walikuwa wanadai kiwango cha Chalobah ni sawa na Bakayoko, alijibu "Chalobah ni mchezaji mzuri lakini sio wa kufananishwa na Bakayoko. Hajacheza michezo mingi kama Bakayoko, hajacheza Uefa kama Bakayoko, kwa maana hiyo Bakayoko bado ana uwezo mkubwa kuliko Chalobah"

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.