Tuesday, 25 July 2017

Usajili umekamilika; Izzy Brown atimkia Brighton

Mshambuliaji kinda wa Chelsea, Izzy Brown nae ametimkia klabu ya Brighton & Hove Albion iliyopanda daraja kutokea daraja la kwanza Uingereza maarufu kama Championship na msimu ujao itacheza ligi kuu Uingereza maarufu kama Premier League.

Kinda huyo mwenye miaka 20 aliyejiunga na Chelsea toka 2013 amejiunga na klabu hiyo aliyoitumikia msimu uliopita kwa mkopo wa muda mrefu yaani atarudi tena Chelsea mpaka msimu uishe labda aitajike na kocha. Lakini wakati anajiunga na klabu hiyo ameshasaini mkataba mpya na Chelsea wa miaka minne.

Izzy Brown anaongeza idadi ya wachezaji wa Chelsea wanaocheza klabu inayoshiriki ligi moja na klabu hiyo mtindo ambao mwandishi mmoja aliyestaafu wa Sky Sports aliilalamikia na kusema mtindo huo unadhoofisha utamu wa ligi.

Wachezaji wengine waliotolewa kwa mkopo na klabu hiyo wanaochezea timu zinazoshiriki ligi kuu ni;
-Ruben Loftus-cheek aliyejiunga na Crystal Palace kwa mkopo
-Kasey Palmer aliyejiunga na Huddersfield
-Kurt Zouma aliyejiunga na Stoke city
-Tammy Abraham aliyejiunga na Swansea

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.