Tuesday, 25 July 2017

Kennedy bado anafatiliwa

Mchezaji kinda wa Chelsea, Robert Kennedy ambae ni raia wa Brazil amekuwa na majanga safari hii mara baada ya kutuma ujumbe ulioonyesha kuwazalilisha wananchi wachina.

Mchezaji huyo alituma katika mtandao wa China habari ambayo ilionyesha udhalilishaji ambapo Chelsea ilifika nchini humo kwa dhiara ya kujiandaa na msimu mpya.

Baada ya kusolewa sana na wananchi wa taifa hilo mchezaji huyo aliomba msamaha lakini pia klabu nayo ikaomba msamaha kwa kitendo kilichofanywa na mchezaji huyo.

Lakini baada ya kitendo hicho kumeinuka rungu jengine kwake mara baada ya chama cha soka nchini Uingereza, FA kuanza kufanya uchunguzi kwa kitendo hicho alichokifanya na kama ikijilizisha kwamba kweli alifanya makosa basi huenda akapata adhabu kali.

Mchezaji huyo pia hakujumuishwa kabisa kwenye mchezo wa leo dhidi ya Bayern Munich na kama hio haitoshi imeamliwa mchezaji huyo arudishwa Uingereza na ataisubiri timu huko.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.