Tuesday, 25 July 2017

Morata vs Bayern Munich

Alvaro Morata hatimaye amecheza katika mchezo wake wa kwanza jioni ya leo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bayern Munich katika mchezo ambao Chelsea ilikufa kwa mabao 3-2.

Morata ambae alisajiliwa siku kadhaa zilizopita na klabu yake mpya ya Chelsea kwa dau lililomfanya kuwa mhispania ghali zaidi baada ya Chelsea kutoa kiasi cha paundi milioni 70 dau ambalo limeivunja rekodi ya mhispania mwenzake Fernando Torres aliyesajiliwa na klabu hiyo hiyo ya matajiri wa jiji la London.

Mchezaji huyo amepewa nyota 5/10 na vyombo vingi vya habari vya michezo vikitoa maoni kwamba sio mwanzo mbaya kwa mchezaji huyo.

Antonio Conte ambaye ni kocha wa Chelsea ametoa pia maoni yake juu ya mchezaji huyo akisema "sio mwanzo mbaya anahitaji muda zaidi wa kuzoea jinsi tunavyocheza"

Lakini pia mchezaji huyo kwenye mtandao wa Instagram ametuma picha huku akieleza amefurahi kuichezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza na yupo tayari kufanya kazi kwa jitihada kubwa zaidi.

Mchezaji huyo ameingia kwenye mchezo huo katika dakika ya 65 akichukua nafasi ya kinda Jeremie Boga.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.