Saturday, 1 July 2017

Usajili ndani ya Chelsea mpaka sasa

Mpaka sasa bado hakuna mchezaji aliyesajiliwa ndani ya Chelsea wakati ikitegemewa kwamba kikosi cha Chelsea inabidi kiimalike kuelekea msimu mpya wa 2017-2018.
Lakini kuna wachezaji watatu waliokuwa wanatajwa na bado inaonekana kuna asilimia kubwa kwa sajili hizo zikatimia kabla ya wiki inayoanza jumatatu kuisha.
Alex Sandro, ni beki wa kushoto anayetajwa na kuhusishwa kwa karibu kwamba muda wowote anaweza akatua ndani ya Chelsea tena kwa dau kubwa linalotazamiwa kufikia £61.5milioni. Akitokea Juventus.
Tiemou Bakayoko, kinda huyu mwenye uraia wa Ufaransa anatajwa kwa karibu kutua Chelsea na kutengeneza kiungo imara na mfaransa mwenzake N'golo Kante. Thamani yake inatajwa kufikia £35milioni akitokea Monaco ambao ni mabingwa wa Ligue 1.
Antonio Rudiger, huyu ameingia kwenye rada za Chelsea muda mfupi tu akitazamiwa kutua Chelsea kuwa mrithi wa mkongwe, John Terry. Rudiger ambaye ni raia wa Ujerumani anayekiputa As Roma ya Italia anatajwa kuwa na uwezo mkubwa katika kukaba na kupiga pasi ndefu ambapo msimu wa 2016-2017 amekuwa ndie beki aliyepiga pasi za mipira mirefu mingi kuliko beki yoyote katika ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A. Thamani yake inatajwa kuwa ni £30milioni.
Hapa chini nimekuwekea video ya Antonio Rudiger na uwezo wake kama mlinzi bora...

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.