Tuesday, 25 July 2017

Stoke city washindana na Chelsea

Klabu ya Stoke city huenda ikaipiku Chelsea juu ya mchezaji Chamberlan. Taarifa zilizopo ni kwamba timu hiyo imeanza mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo anayeichezea Arsenal na inaonekana mazungumzo baina ya pande hizo yanaendelea vizuri.

Alex-Oxlade Chamberlain anatajwa kukataa kuongeza mkataba katika klabu hiyo ya washika bunduki wa London ambapo mkataba wake na klabu hiyo unaisha kipindi cha kiangazi msimu ujao.

Thamani ya mchezaji huyo inatajwa kufikia kiasi cha paundi milioni 25. Na kwa inavyotaarifiwa Arsene Wenger, kocha wa Arsenal anaweza akakubali ofa ya kumuuza mchezaji huyo kwenda Stoke city maana kocha huyo hataki kumuuza mchezaji kwa timu anayoshindana nayo kwenye kuwania mataji.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.