Haya sasa. Baada ya kuwepo tetesi za muda mrefu juu ya mbrazili Alex Sandro kuhusu kutakiwa kwa karibu na mabingwa wa Uingereza, Chelsea sasa mambo yanaonekana kwenda vizuri baada ya kuwepo vikwazo mbalimbali vilivyowekwa na mabingwa wa Italia, Juventus ambayo ndio klabu inayommiliki mchezaji huyo.
Mlinzi huyo wa kushoto ambaye inaelezwa kwamba yeye anataka kujiunga na Chelsea ingawa vikwazo viliwekwa na vibibi vya Turin maarufu kama Juventus ingawa imetoka taarifa mpya kwamba makubaliano juu ya usajili wa mchezaji huyo yatafanyika kesho jumatatu. Ambapo inaonyesha Juventus kwa asilimia kubwa watakubali kumuuza kwa kutamanishwa na dau ambalo Chelsea wameweka ambapo Chelsea imesema ipo tayari kutoa kiasi cha paundimilioni 60.

No comments:
Post a Comment