Beki mahiri wa AS Roma ambaye usiku wa jana aliiongoza timu yake ya taifa ya Ujerumani ilimenyana na Chile katika fainali ya kombe la FIFA Cofederation ameonyesha nia yake ya dhati kwa msimu ujao atatua Chelsea.
Hiyo imedhihirika katika mtandao wa Instagram ambapo rafiki wa mchezaji huyo alituma picha akiwa na Rudiger nakuandika "Hongera Rudiger, kituo kinachofata ni Chelsea" alafu picha hiyo kupendezwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.
Rudiger amekubaliana na Chelsea ili kutua katika klabu hiyo. Wakati huohuo klabu ya Manchester city imesema nayo inataka kushindana na Chelsea katika kumuwania mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment