Mchezaji mjerumani aliyesajiliwa kutokea AS Roma, Antonio Rudiger ataanza katika kikosi cha leo kitakachocheza dhidi ya Inter Milan katika mchezo wa kirafiki nchini Singapore.
Antonio Conte alipoojiwa kuhusu mchezo huo alisema atawachezesha wachezaji wote wa kikosi cha kwanza ili kupata zoezi kwa kikosi hicho kuelekea mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Arsenal tarehe 06-Agosti.
Mpaka sasa wachezaji waliosajiliwa katika dirisha kubwa la usajili ni Alvaro Morata na Willy Caballero tu waliocheza katika michezo ya kirafiki. Tiemoue Bakayoko ambaye naye alisajiliwa akitokea AS Monaco ana majeruhi yanayomfanya kukaa nje mpaka ligi itakapoanza tarehe 12-Agosti.
No comments:
Post a Comment