Kocha Antonio Conte bado hajatulia kabisa, na hajaridhika katika usajili hii ni mara baada ya kuhusishwa na wachezaji waingereza.
Ross Barkley na Alex Oxlade Chamberlain wote wanatajwa kuwaniwa na Antonio Conte ambaye anajipanga kulinda taji lake la ligi kuu Uingereza alilolitwaa katika msimu wake wa kwanza Uingereza.
Barkley wa Everton anatajwa sana katika dili hili ambapo Conte anamfukuzia kwa karibu kijana huyu ambaye katika mkataba wake amebakiza miezi 12 ambao ndo sawa na mwaka mmoja, huku mwingereza mwenzake pia Chamberlain nae akizidi kuipa presha klabu yake ya sasa, Arsenal.
Chamberlain nae kabakiza miezi 12 kwenye mkataba wake na ameshakataa ofa ya kusaini mkataba mpya.
No comments:
Post a Comment