Saturday, 29 July 2017

Pochettino awakata maini Man utd

Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino ambaye ni raia wa Argentina amewakata maini Manchester united ambao walikuwa wanaifukuzia saini ya nyota wa klabu hiyo, Dier.

Pochettino amesema "ni jambo zuri kusikia nyota wa Tottenham wakitajwa kutakiwa na klabu nyengine. Lakini hizo zitabaki kuwa tetesi tu"

Alisema kocha huyo ambapo mchezaji nyota wa klabu yake mwenye uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji au mlinzi wa kati amekuwa akitakiwa kwa karibu na Mourinho ili akaungane nae klabuni Manchester united.

Lakini pia kocha huyo amewatoa hofu mashabiki wanaofikiria au wanaoshangazwa na klabu hiyo juu ya kutokufanya usajili wowote mkubwa mpaka sasa na kocha huyo amesema hilo halina tatizo kama akihitaji kufanya usajili basi atafanya lakini kwa sasa anawaamini wachezaji wake.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.