Mchana wa leo kuna mchezo wa kirafiki ambapo Chelsea itashuka uwanjani katika mchezo wa nne wa kirafiki ambapo itamenyana na wababe wa jiji la Mila, Inter Milan.
Mchana wa saa 14:45 ndo mchezo utaanza na Conte amepanga kupanga kikosi ambacho huenda atakitumia katika mchezo dhidi ya Arsenal katika ufunguzi rasmi wa ligi kuu Uingereza, mchezo wa ngao ya hisani.
Antonio Conte ambaye mchezo uliopita aliishuhudia timu yake ikipoteza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Bayern Munich kwa mabao 3-2 lakini Bayern Munich huyohuyo akabamizwa na Inter Milan mabao 2-0.
Kikosi cha leo kinaweza kuwa hivi hapo kwenye picha ambapo Conte amebadilisha mfumo wake wa kawaida kutoka 3-4-3 mpaka 3-5-2.
No comments:
Post a Comment