Saturday, 29 July 2017

Conte kuvuta nyota wengine

Licha ya kuvuta nyota wanne ambao ni Morata, Rudiger, Bakayoko na Caballero lakini bado inaelezwa Antonio Conte anataka kuongeza nyota wengine wawili.

Gazeti la Uingereza, Dailymail linaeleza bado kuna uwezekano wa Conte kutumia fungu alilopewa na mmiliki wa klabu kuweza kuwasajili Alex Sandro anayetajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 61 wakati pia kocha huyo anamtaka mshambuliaji aliyewai kufanya nae kazi wakiwa Juventus, Fernando Llorente anayetajwa kufikia paundi milioni 20 anayeichezea Swansea kwa sasa.

Gazeti hilo linaeleza licha ya Juventus kuweka ngumu kumuuza mchezaji wao Alex Sandro aliyeisaidia klabu hiyo kutwaa taji la ligi kuu Italia na kufika fainali ya ligi ya mabingwa ulaya, lakini bado Antonio Conte anaonekana kutokata tamaa na anaendelea kupeleka fungu la ela ili kumsajili mchezaji huyo.

Lakini pia Conte anatajwa kuwafukuzia kwa karibu Ross Barkley wa Everton, Oxlade Chamberlain wa Arsenal na Renato Sanches wa Bayern Munich anayetajwa kupatikana kwa mkopo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.