Kocha wa mashetani wekundu, Jose Mourinho ameeleza sababu ya kuachana na mpango wa kumrudisha kundini mshambuliaji wa klabu hiyo, Javier Hernandez 'Chicharito'.
Jose Mourinho alipoulizwa alijibu "sababu ya kwanini niliachana na Chicharito kwa vile sikujua wakati alipoondoka hapa miaka kadhaa nyuma aliondoka kwa hitaji lake au kocha ndo alitaka aondoke"
Kocha huyo mwenye maneno mengi siku ya leo atakuwa na mchezo mwengine wa kirafiki ambapo atamenyana na Barcelona katika mchezo wa kirafiki.
No comments:
Post a Comment