Mechi imeisha, Chelsea tumefungwa 3-2 na Bayern Munich.
Magoli yakifungwa na Rafinha wa Bayern Munich katika dakika ya 6 kabla ya Thomas Muller kufunga mara mbili. Wakati ikielekea mapumziko Victor Moses akapiga krosi tamu iliyomkuta Marcos Alonso na kufumua shuti kali lililomshinda kipa wa Bayern Munich.
Kipindi cha pili kilianza kasi kabla ya kufanyika mabadiliko, Alvaro Morata akivaa jezi kwa mara ya kwanza yenye namba 9 mgongoni akiingia kuchukua nafasi ya Jeremie Boga.
Christensen kinda aliyekuwa anaichezea Borrusia Monchnglebach kwa mkopo aliyeanza kwenye mchezo huu akatoka na nafasi yake kuchukuliwa na David Luiz.
Mabadiliko hayo ni kama zilisaidia ambapo Chelsea ilifanya mashambulizi kadhaa baadae ukapatikana mpira wa kona uliopigwa na Cesc Fabregas na kuunganishwa na Gary Cahill kabla ya Batshuayi kufunga kwa goli safi na kufanya mpira kuisha kwa mabao 3-2.
No comments:
Post a Comment