Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Alan Smith ameipa bingo klabu ya Chelsea kwa kumsajili Alvaro Morata licha ya kumkosa Romelu Lukaku.
Alan Smith alisema "Chelsea itakuwa klabu ya kuogopwa maana imempata mtu sahihi (Morata), naamini ni chaguo sahihi kuliko hata wangemsajili Lukaku"
Chelsea ilimsajili Morata akitokea Real Madrid mara baada ya biashara ya kumsajili Lukaku kwenda tofauti na mchezaji huyo kujiunga na Man utd.
Morata alicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Bayern Munich ulioshuhudiwa klabu yake ikifungwa 3-2 ikiwa katika ziara barani Asia.
No comments:
Post a Comment