Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesema hataki kufanya haraka kuwarudisha uwanjani wachezaji Eden Hazard na Tiemoue Bakayoko.
Conte alihojiwa kuhusu uwezekano wa wachezaji hao kuwai kurudi uwanjani kutokana na kuwa na majeraha lakini Antonio Conte alisema ni kweli tunawahitaji lakini hatuwezi kuwarudisha kwa haraka, cha muhimu ni wapone kabisa kisha ndo waungane tena na timu.
Eden Hazard aliumia akiwa anaitumikia timu ya taifa ya Ubelgiji wakati Bakayoko alisajiliwa akitokea Monaco kwa ada ya paundi milioni 40 akiwa na majeruhi.
No comments:
Post a Comment