Mabingwa wa ligi kuu Uingereza, Chelsea bado inaendelea kuifukuzia saini ya mlinzi wa kushoto wa Juventus, Alex Sandro.
Chelsea imejiandaa kutoa kiasi cha paundi milioni 61 ili kumsajili mchezaji huyo mwenye uraia wa Brazil na mpango huo umekuwa unachukua muda mrefu kukamilika.
Conte inadaiwa kapokea fungu tosha la zaidi ya paundi milioni 150 kutoka kwa mmliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich ili afanye usajili wa nguvu kabla kuanza msimu mpya.
Mpaka sasa Antonio Conte ashawavuta Alvaro Morata kwa dau la paundi milioni 70, Tiemoue Bakayoko kwa dau la paundi milioni 40, Antonio Rudiger kwa paundi milioni 34 na Willy Caballero aliyesajiliwa bure akitokea Manchester city.
No comments:
Post a Comment