Jina kamili; Antonio Conte
Tarehe ya kuzaliwa; 31-07-1969 (Miaka 48)
Mahali alipozaliwa; Lecce, Italia
Urefu; mita 1.78 (futi 5 na inchi 10)
Kwa sasa; Ni kocha wa Chelsea
Maisha yake kama mchezaji;
Alianza kuichezea klabu ya jijini kwao Lecce mwaka 1985 akiwa na miaka 15 katika akademi ya kukuzia vipaji na kupandishwa mpaka timu ya wakubwa akiwa kama kiungo wa kati akaichezea Lecce michezo 71 na kuifungia goli 1.
Mwaka 1991 aliachana na Lecce na kujiunga na Juventus aliyoichezea kwa mafanikio makubwa ambapo miaka 5 baadae akachaguliwa kuwa nahodha wa Juventus na kocha Marcello Lippi ambaye kwa sasa anaifundisha klabu huko nchini China. Na aliichezea Juventus michezo 296 na kuifungia magoli 29 huku akiiongoza kutwaa taji la ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A mara 5 na kombe la ligi ya mabingwa ulaya maarufu kama Uefa Champions League mara moja. Kumbuka pia wakati akiwa Juventus alishawai kuwa nahodha mbele ya nyota kama Zinedine Zidane.
Wakati akiwa Juventus alitumia miaka 3 tu kukubalika na kuingia katika kikosi cha timu ya taifa ya nchini kwao Italia, ambayo aliichezea toka mwaka 1994 mpaka 2000 na kuichezea michezo 20 na kuifungia magoli 2.
Maisha yake kama kocha;
Alianza harakati za ukocha akizifundisha klabu kadhaa nchini kwao Italia, akianza na Arezzo aliyoifundisha mwaka 2006 mpaka 2007 kabla ya kumwaga wino kuifundisha klabu ya ligi daraja la kwanza nchini Italia maarufu kama Serie B, klabu ya Bari.
Atalanta ikamchukua kama kocha na kuifundisha toka mwaka 2009 mpaka 2010 ambapo aliungana tena na Siena.
Mafanikio yake katika ukocha yalionekana zaidi baada ya kujiunga na Juventus ambapo alianza nayo mwaka 2011 na kuitambulisha mfumo wa 3-5-2 ambao ulikuwa maarufu na kuiwezesha klabu hiyo ya Turin kupata mafanikio makubwa akiisaidia kutwaa taji la ligi kuu Italia maarufu kama Serie A mara 3.
Baada ya kuiongoza timu ya taifa ya Italia kama kocha katika michuano ya Euro 2016 akatangazwa rasmi kujiunga na Chelsea tarehe 04-Aprili-2016 na kusaini mkataba wa miaka 3.
Alipotua Chelsea wengi hawakuzani kama angeisaidia klabu hiyo kurudi katika makali yake mara baada ya msimu uliopita klabu hiyo kuwa na kiwango kibovu na kushuhudiwa ikimaliza nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu Uingereza.
Alipofika klabuni hapo katika michezo ya ligi kuu alianza West Ham lakini alifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1. Mpaka ligi inaisha tarehe 21-05-2017, Chelsea ilitangazwa rasmi kuwa bingwa wa ligi hiyo na kufanikiwa kuweka na kuvunja rekodi kadhaa kama ya kuweka rekodi ya kushinda michezo 30 kwa msimu mmoja ikiwa ndio klabu ya kwanza kufanya hivyo kwa ligi hiyo.
Mafanikio yake mpaka sasa klabuni hapo ameisaidia Chelsea kutwaa ligi kuu ya Uingereza na kuifikisha klabu hiyo fainali ya kombe FA lakini pia akachaguliwa kuwa kocha bora wa msimu nchini Uingereza.
Antonio Conte ni mme wa mke mmoja na mtoto mmoja wa kike.
Jambo usilolijua kuhusu muitaliano huyu, aliwai kuingia kwenye kesi ya kubashiri au kupanga matokeo alipokuwa katika klabu moja huko Italia akiwa kama kocha. Mmiliki wa klabu ambayo Conte alikuwa akiifundisha, aliwekeana kidau na mwenzake na mmiliki huyo akatabiri mchezo wa klabu yake na klabu nyengine itaisha kwa suluhu, baada ya kuwekeana dau hilo tajiri huyo akawapigia wachezaji wake na kuwaambia wacheze watakavyocheza ila mchezo huo lazima uishe kwa suluhu. Na kweli ukaisha kwa suluhu ya 2-2.
Lakini ilipofanyika uchunguzi ikagundulika na moja wa wachezaji akamshtumu Antonio Conte kwamba nae amehusika katika upangaji matokeo hayo.
No comments:
Post a Comment