Monday, 31 July 2017

Mjue zaidi Charly Musonda Jr.

Jina kamili; Charles Musonda
Tarehe ya kuzaliwa; 10-Oktoba-1996 (miaka 22)
Mahali alipozaliwa; Brussels, Ubelgiji
Urefu; mita 1.73 (futi 5 na inchi 8)
Nafasi anayocheza; Kiungo mshambuliaji au Winga
Timu aliyopo; Chelsea
Jezi namba; 17

Maisha yake ya soka;
Charles Musonda au Charly Musonda Jr. ni kinda mwenye asili ya Zambia ambapo ndio asili ya baba yake mzee Charles Musonda.

Alianza kucheza soka akiwa na miaka 15 katika akademi au shule ya kukuza vipaji ya Anderlecht, klabu ambayo baba yake alishawai kuichezea.

Wakati akiwa na umri huo tayari kipaji chake kilionekana na klabu kama Real Madrid na Barcelona zilishapeleka ofa ili kumsajili kinda huyo, lakini maskauti wa Chelsea wakashinda vita hiyo na kumtwaa kinda huyo mwenye mbwembwe nyingi kwenye kuuchezea mpira. Hiyo ilikuwa mwaka 2012.

Alicheza kwenye akademi ya Chelsea kwa muda mrefu mpaka mwaka 2015 alipopandishwa mpaka kikosi cha wakubwa ingawa hakufanikiwa kupenyeza kwenye kikosi cha kwanza na kucheza mchezo wowote katika timu ya wakubwa.

Baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha wakubwa ambapo kwa kipindi hicho ilikuwa chini ya Jose Mourinho akatolewa kwa mkopo na kwenda Real Betis ya Hispania, hiyo ilikuwa 2016.

Alipojiunga na klabu hiyo ya Real Betis alifanikiwa kuichezea michezo 24 ambapo katika mchezo wake wa kwanza akiwa klabuni hapo, aliiongoza klabu hiyo kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Valencia na Musonda akachaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo.

Siku 6 baadae katika mchezo dhidi ya Deportivo La Coruna alifunga goli lake la kwanza kama mchezaji wa kulipwa katika mchezo ulioisha kwa suluhu ya 2-2.

Lakini baada ya safari yote hiyo, kocha Antonio Conte akamrudisha kikosini ambapo mchezo wake wa kwanza kucheza katika timu ya wakubwa akiwa Chelsea ni ule wa kirafiki uliochezwa nchini Singapore dhidi ya Inter Milan akiingia kama mchezaji wa akiba na Chelsea ilipoteza kwa 2-1.

Huyu ndio Charles Musonda Jr., labda usilolijua kuhusu Musonda wakati akijiunga na Chelsea alijiunga pamoja na ndugu zake, ambapo aliongozana na kaka zake Lamisha na Tika na mdogo wake Matty ambao na wao walijiunga katika akademi ya Chelsea.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.