Jina kamili; John George Terry
Tarehe ya kuzaliwa; 07/12/1980 (miaka 36)
Alipozaliwa; Barking, London, Uingereza
Urefu; meta 1.87
Nafasi anayocheza; Mlinzi wa kati
Namba ya fulana; 26
Tarehe ya kuzaliwa; 07/12/1980 (miaka 36)
Alipozaliwa; Barking, London, Uingereza
Urefu; meta 1.87
Nafasi anayocheza; Mlinzi wa kati
Namba ya fulana; 26
John Terry alianza kucheza soka ambalo sio rasmi (bila mkataba) katika kituo cha Eastbury Comprehensive School ambapo alisajiliwa rasmi katika kituo cha kukuza vipaji cha West Ham United mwaka 1991 akiwa anacheza nafasi ya kiungo wa kati.
Alicheza hapo kwa mafanikio akionyesha kipaji cha hali ya juu kabla kabla ya kujiunga na Chelsea akiwa na miaka 14 hapo ikiwa mwaka 1995. Alicheza katika kituo cha Chelsea kabla ya msimu wa 1998 kupandishwa katika timu ya wakubwa akiwa kama mlinzi wa kati ambapo alijifunza kuichezea nafasi hiyo baada ya kuhamishwa nafasi akiwa katika akademi ambapo kutokana na uchache wa walinzi wa kati basi Terry ndio akatumika kuanzia hapo akiwa ndie mlinzi wa kati.
Alicheza ndani ya Chelsea kabla ya kutolewa kwa mkopo na kwenda kuichezea Nottingham Forest msimu wa 1999/2000 ambapo huko alicheza michezo 6 huku akicheza kwa ustadi mkubwa kabla ya Chelsea kumrudisha tena ambapo mwaka huo wa 2000 alifanikiwa kuchaguliwa kujiunga na timu ya taifa ya Uingereza ya chini ya miaka 21 maarufu kama England U-21.
Mchezo wake wa kwanza kuichezea Chelsea ya wakubwa ilikuwa tarehe 28-10-1998 alipoingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Aston Villa klabu ambayo sasa imetangazwa na rais wa klabu hiyo kwamba ataichezea kwenye msimu wa 2017-2018 ambapo amesajiliwa na klabu hiyo kama mchezaji huru.
Baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba siku kadhaa baadae katika msimu huohuo alifanikiwa kuichezea Chelsea mchezo wake wa kwanza akiwa katika 'first eleven' ya Chelsea katika mchezo dhidi ya Charlton Albion ambao ulikuwa mchezo wa kombe la FA wa raundi ya tatu ambapo Chelsea ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0.
Alifanya vizuri na kung'aa na katika msimu wa 2001-2002 alifanikiwa kucheza michezo 23 ikiwa ni dalili nzuri kwake katika safari ya mafanikio huku Claudio Ranieri aliyekuwa kocha wa Chelsea kipindi hicho akimkabidhi kitambaa cha unahodha katika mchezo dhidi ya Charlton Albions ambapo nahodha mkuu wa kipindi hicho, Marcel Desailly alipokosekana kwenye timu na hiyo ndio kama ilimpa mwanga wa kuwa kiongozi bora.
Mwaka 2002 ulikuwa mbaya kwa John Terry ambapo alishitakiwa kwa kufanya vurugu dhidi ya mlinzi wa kumbi moja ya usiku akiwa na mchezaji mwenzake wa Chelsea ambapo hali hiyo ilimfanya afungiwe na Chama Cha Soka cha Uingereza (FA) kuichezea timu ya taifa ya Uingereza.
Tukivuka miaka na matukio kibao, tunadondokea tarehe 14-10-2006 ambapo John Terry ilibidi awe mlinda mlango (goalkeeper) mara baada ya makipa wa Chelsea, Carlo Cudicini na Petr Cech kipindi hicho walipopata majeraha na hivyo kumlazimu kocha, Jose Mourinho kumchagua Terry akakae kipa. Hii ilikuwa katika mchezo dhidi ya Reading ambapo mchezo uliisha kwa Chelsea kupata ushindi wa 1-0.
Lakini pia mwaka huohuo mwezi mmoja baadae John Terry alitolewa nje kwa mara ya kwanza na mwamuzi baada ya kupata kadi mbili za njano katika mchezo ambao Chelsea ilipoteza dhidi ya Tottenham katika uwanja wa White Hart Lane ambapo ndo ilikuwa mara ya kwanza Tottenham kupata ushindi uwanjani hapo toka mwaka 1987 dhidi ya Chelsea.
Tukivuka siku na miaka mingi mpaka tarehe 17-04-2017 itabaki kuwa siku ya kukumbukwa kwa wapenzi na mashabiki wa Chelsea mara baada ya nguli huyo kutangaza rasmi kwamba ataachana na Chelsea rasmi ufikapo mwisho wa msimu.
21-5-2017 katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Uingereza katika uwanja wa Stamford Bridge, mnamo dakika ya 26 ya mchezo wa siku hiyo wa kufunga ligi John Terry lilionyeshwa bango na kuonyesha mchezaji aliyevaa jezi namba 26 (John Terry) anatakiwa kutoka ambapo alitumia dakika 2 kuwaaga mashabiki huku akitoka uwanjani kwa heshima kubwa jipita katikatibya waxhezaji wa Chelsea waliomeachia nafasi katikati yao. Hii ndo ilimaanisha John Terry rasmi kwamba hatovaa jezi za Chelsea akiwa kama mchezaji. Lakini aliachana na klabu hiyo akiwa na historia kubwa ndani ya Chelsea akiwa ndie nahodha aliyeipatia klabu hiyo mataji mengi kuliko nahodha yoyote.
Amefanikiwa kuichezea Chelsea michezo 717 akiifungia magoli 67 akiwa ndie mlinzi aliyefunga magoli mengi Uingereza. Huku kwa upande wa timu yake ya taifa ya Uingereza aliichezea michezo 78 na kuifungia magoli 6.
Tarehe 15-06-2007 alifunga ndoa na mke wake, Toni (nee Poole) aliyezaa nae watoto mapacha Georgio John na Summer Rose waliozaliwa 18-05-2006.
Mataji aliyotwaa akiwa Chelsea ni Ligi kuu ya Uingereza (EPL) mara 5, FA Cup mara 5, Kombe la Ligi mara 3, Uefa Champions League mara 1 na kombe la Ueropa League mara 1.
No comments:
Post a Comment