Ni habari itakayomgusa kila shabiki wa Chelsea lakini hata kwa kila mpenda soka mara baada ya rais wa klabu ya Aston Villa kuitangazia dunia kwamba mkongwe wa Chelsea, John Terry amemwaga wino katika klabu yake.
John Terry ambaye ameichezea Chelsea kwa miaka 22 na miaka 14 akiwa kama nahodha wa klabu hiyo anajiunga na klabu hiyo akiwa amecheza kwa mafanikio makubwa akiwa ndie nahodha aliyebeba makombe au mataji 5 ya Ligi Kuu Uingereza maarufu kama Premier League anajiunga na klabu hiyo ya Aston Villa mara baada ya kutangaza ataachana na Chelsea ili kuwaachia vijana waweze kupata nafasi ya kucheza. Terry au JT amejiunga na Aston Villa baada ya kumaliza mkataba na mabingwa wa Uingereza na kwa maana hiyo amejiunga na klabu hiyo bure.
Ana historia kubwa katika soka la Uingereza na dunia pia huku akiwa mlinzi aliyefunga magoli mengi, zaidi ya magoli 60. Na kama haujajua John Terry hakuwai kuichezea klabu yoyote rasmi zaidi ya Chelsea ukiondoa ile klabu ya Nottingham Forest ambayo aliichezea kwa mkopo akitokea Chelsea.
Kwaheri Shujaa wetu...
Na nitakuletea historia ya maisha ya John Terry.
Na nitakuletea historia ya maisha ya John Terry.
No comments:
Post a Comment