Huenda chelseatz1905.blogspot.com ikawa ndo blog ya kwanza ya kiswahili kuandika taarifa hii.
Nyota wa Barcelona, Lionel Messi amemuaga muamerika kusini mwenzake mwenye uraia was Brazil, Neymar Jr.
Neymar anahusishwa kwa karibu kutua PSG ambayo wiki kadhaa ilimsajili mbrazili mwengine Dani Alves ambaye pia alishawai kuichezea Barcelona kama Neymar na sasa huenda wabrazili hao wakaungana.
Messi alimuaga nyota huyo katika mchezo wa El Classico uliochezwa juzi katika mji wa Miami ambapo Barcelona iliikung'uta Real Madrid mabao 3-2.
Na Messi kuonyesha kwamba ni kama ashakubaliana na Neymar kuondoka klabuni hapo amewachagua Paulo Dybala wa Juventus na Phillip Coutinho wa Liverpool kwamba mmojawapo asajiliwe ili kuziba pengo la nyota huyo.
No comments:
Post a Comment