Nyota wa Tottenham, Harry Kane amemjibu kocha wa Chelsea, Antonio Conte baada ya kocha huyo kumsifia mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita alikuwa mfungaji bora.
Antonio Conte alitoa maneno ya kumsifia mshambuliaji huyo mara baada ya kusema kama angetakiwa kumsajili mshambuliaji, basi angemsajili nyota huyo raia wa Uingereza. Na huku akizidisha sifa kwa mshambuliaji huyo mara baada ya kusema, ni mzuri juu na hata anacheza na kufunga magoli ya kila aina.
Antonio Conte amefanikiwa kumnasa nyota wa kihispania, Alvaro Morata atakayekuwa mshambuliaji wa kati mara baada ya Diego Costa kuonyeshwa mlango wa kutokea.
Mshambuliaji huyo alijibu kwa kusema "ni maneno mazuri kuyasikia, lakini jambo la muhimu kwa sasa ni kumsikiliza kocha wangu (wa Tottenham) nini anataka kuelekea msimu mpya."
Lakini pia kabla ya mshambuliaji huyo kutoa majibu hayo, kocha wake wa Tottenham raia wa Argentina, Mauricio Pochettino alijibu maneno hayo kabla ya mshambuliaji huyo kutoa majibu, alisema "nashangaa kwanini makocha wa timu nyengine wanaitazama sana timu yangu"

No comments:
Post a Comment