Saturday, 29 July 2017

Mbwembwe za Conte zampa majanga

Kocha wa Chelsea ambaye anajulikana kwa mbwembwe za ushangiliaji wake kwa msimu uliopita alipoiongoza klabu hiyo kutwaa taji la ligi kuu Uingereza. Sasa zile mbwembwe zake zimempa matatizo na anaweza akapunguza.
Conte alikaririwa akisema msimu uliopita alikuwa anashangilia sana tena kwa mbwembwe nyingi zilizomfanya uzito wake upungue kwa kilo mbili kuliko ule uzito aliofika nao klabuni hapo akitokea timu ya taifa ya Italia aliyokuwa anaifundisha kama kocha mkuu.
Lakini pia kocha huyo aliwai kusikika akisema zile mbwembwe za ushangiliaji wake huwa anazifanya bila kujijua na sio kama huwa anapanga kushangilia vile, ila anajikuta tu ashashangilia.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.