Kiungo wa Chelsea raia wa Serbia, Nemanja Matic atajwa kugombaniwa na klabu tatu ambazo ni Man utd, Inter Milan lakini pia na Juventus.
Nyota huyo hajaungana na wenzake katika kujiandaa na msimu mpya barani Asia na badala yake amekuwa akifanya mazoezi peke yake akiusishwa na kuondoka klabuni hapo.
Manchester united ndo wanaonekana kuongoza katika mbio hizo ambapo kocha wa timu hiyo Jose Mourinho anataka kuungana na nyota huyo waliofanya kazi wote pindi Mourinho alipokuwa anaifundisha Chelsea.
No comments:
Post a Comment