Wednesday, 26 July 2017

Conte ajazwa mapesa na Roman

Kocha Antonio Conte sasa amekabiziwa kitita cha pesa rasmi ili afanye usajili mkubwa katika kampeni za kuijenga timu kuelekea msimu mpya.

Kocha huyo amepokea kitita cha zaidi ya paundi milioni 140 baada ya kumshawishi mmiliki wa klabu hiyo ya Chelsea, Roman Abramovich ili afanye usajili mkubwa kuelekea msimu atakaoiongoza Chelsea katika michuano mingi.

Kocha Antonio Conte baada ya kupata muhamala huo ameanza na jitihada za kumsajili kinda wa Everton, Tom Davies mwenye miaka 19 na anataka kumsajili kinda huyo huku kukiwa na tetesi za kiungo wake Nemanja Matic kukaribia kuondoka.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.