Sunday, 30 July 2017

Matic ang'ang'ania kuondoka

Nyota wa Chelsea, kiungo mkabaji Nemanja Matic amepiga picha akiwa na jezi ya Manchester united inayonolewa na kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho.

Nyota huyo ambaye amekuwa hana muendelezo mzuri klabuni kwake, Chelsea aliyoisaidia kutwaa taji la ligi kuu Uingereza mara mbili katika misimu mitatu.

Kiungo huyo mwenye uraia wa Serbia pia hakusafiri na timu kwenda ziarani barani Asia ambapo alibaki London akifanya mazoezi peke yake, mchezaji huyo ambaye amekuwa akiusishwa na kujiunga na kocha wake wa zamani ambaye walifanya kazi wakati kocha huyo akiwa Chelsea.

Lakini Chelsea inasemekana haitaki kumuuza kiungo huyo mpaka itakapofanikiwa kupata saini ya kiungo mwengine ingawa mapema hii ilifanikiwa kumsajili nyota wa kifaransa Tiemoue Bakayoko.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.