Kocha wa Inter Milan, Luciano Spaletti ambaye leo ameiongoza klabu yake kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Chelsea na kuibamiza klabu hiyo mabao 2-1, lakini kocha huyo hajatosheka na kipigo hicho alichomshushia Antonio Conte, kocha wa Chelsea lakini kambamiza tena nje ya uwanja.
Baada ya mchezo wao kocha Spaletti akahojiwa na waandishi wa habari akasema "Candreva hauzwi. Tunamthamini sana, na kwenye kikosi chetu hakuna wa kuziba nafasi yake" alisema kocha huyo akimuongelea winga wa klabu yake anayefukuziwa kwa karibu na Chelsea.
Antonio Conte anamtaka winga huyo ili kukijenga kikosi kuelekea msimu ambao ataiongoza Chelsea katika mashindano mengi na mechi nyingi.
No comments:
Post a Comment