Sunday, 30 July 2017

Matic 95% ni mali ya Man utd

Nyota na kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic anayehusishwa kutua Manchester united amefanyiwa vipimo na klabu hiyo na kinachosubiriwa kwa sasa ni klabu hiyo kumtangaza mchezaji huyo kuwa ni mali yao.

Kiungo huyo jioni ya leo amepigwa picha akiwa na jezi za Man utd yenye namba 31 ambapo inaelezwa Man utd ipo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 40.

Matic akijiunga na klabu hiyo atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na kocha Jose Mourinho aliyewai kufanya kazi na mchezaji huyo raia wa Serbia wakiwa Chelsea. Nyota wengine waliosajiliwa na klabu hiyo ni Romelu Lukaku na Lindelof.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.