Antonio Conte amempa ushauri nyota mpya wa Chelsea, Alvaro Morata baada ya mchezo wa leo waliopoteza mbele ya Inter Milan kwa mabao 2-1.
Conte amemwambia Morata anahitaji kupambana ili kuonyesha uwezo wake. Lakini pia amtetea na kusema anahitaji muda zaidi kuweza kufanya vizuri mara baada ya kucheza michezo miwili wakati katika mchezo wa kwanza alitoa pasi iliyozaa goli na hii ya leo ameonekana kupotea na kutokufanya vizuri, ingawa kuna mashabiki wamemlaumu Conte kwa kumweka mchezaji huyo upande wa pembeni na kumwacha Batshuayi akicheza kama mshambuliaji wa kati.
Lakini sasa hakuna mchezo mwengine ambao Morata anaweza akajipima maana mchezo unaofata ni dhidi ya Arsenal ambao ni mabingwa wa FA siku ya tarehe 06-Agosti katika uwanja wa Wembley.
No comments:
Post a Comment