Klabu ya Barcelona ambayo inahofu ya kumpoteza nyota wake, Neymar Jr anayetajwa kuwaniwa kwa karibu na PSG na badala yake matajiri hao wa Cataluna wamedai kama nyota huyo akiondoka basi Hazard atatakiwa na klabu hiyo.
Eden Hazard huenda akatupiwa ndoano na wababe hao ambapo pia wanatajwa kuwawania nyota wengine kama Phillip Coutinho wa Liverpool na Delle Alli wa Tottenham.
Hazard kwa sasa anauguza majeruhi yake akiwa jijini London ambapo hajafanikiwa kufanikiwa kusafiri na timu ambayo ipo barani Asia ikimaliza kucheza mchezo wa tatu wa kirafiki mchana wa leo dhidi ya Inter Milan.
No comments:
Post a Comment