Kocha Antonio Conte ambaye amekuwa akilalamikia kuhusu makinda wa klabuni kwake jinsi wanavyoondoka klabuni hapo kwa kuuzwa.
Conte amesema "Kuwa mchezaji kinda sio jambo baya ila ni ngumu kuingia kwenye kikosi cha kwanza kwa haraka inabidi mchezaji akubali kuangaika na kupigana kuonyesha kipaji chake"
"Ni vyema kuwa na wachezaji makinda, na nimewachezesha katika michezo ya kirafiki. Lakini hii itakuwa ngumu kuingia kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza pale Cobham" alisema kocha huyo muitaliano.
"Wakati nilikuwa Juventus sikuweza kuingia kabisa kwenye kikosi cha kwanza na kupigania mataji, ila nilipelekwa Lecce ambapo huko nilipambana" aliongezea kocha huyo ambaye hajafurahishwa na kuondoka kwa makinda wa klabu hiyo kama Nathaniel Chalobah, Dominic Solanke na Nathan Ake.
No comments:
Post a Comment