Mlinzi mpya wa Manchester city ambaye amesajiliwa akitokea Real Madrid, Danilo ameeleza sababu ya kwanini ameikataa Chelsea iliyomfukuzia na kujiunga na Manchester city kwa dau la paundi milioni 26.5.
Mchezaji huyo mlinzi wa kulia alisema "inaeleweka kwamba nimejiunga na Man city na sio Chelsea sababu kubwa nimevutiwa kufanya kazi na Pep"
Aliongezea "wakati nilipokuwa mazoezini na Madrid nilipokea simu kutoka kwa Pep (kocha wa Manchester city) akanishawishi kujiunga na klabu yake. Nilivutiwa na ushawishi wake na nikatamani nifanye nae kazi haraka" alisema mlinzi huyo mwenye uraia wa Brazil.
Lakini mlinzi huyo kujiunga na klabu hiyo atapata upinzani kwa kuwa katika nafasi anayocheza ya mlinzi wa kulia, wamesajiliwa walinzi wengine na kufanya kwenye nafasi hiyo kuwa na watu zaidi ya watatu.
No comments:
Post a Comment