Klabu ya Liverpool imenusurika kupata adhabu kutoka FA ambacho ni chama kinachosimamia soka Uingereza baada ya kuwepo tuhuma za Liverpool kufanya mawasiliano ya kumsajili beki kisiki wa Southampton, Virgil Van Dijk.
Sheria za usajili wa taifa hilo zinakataza timu kufanya mazungumzo ya kumsajili mchezaji ambaye ana mkataba na klabu nyengine bila kufanya mazungumzo na klabu inayommiliki. Mwanzoni mwa mwezi huu Southampton ambayo ina mkataba na beki huyo ililalamika kwa Liverpool wanafanya mazungumzo na beki wao bila kuipa taarifa klabu hiyo iliyopata kocha mpya na kwa hivyo Liverpool ikaomba msamaha kwa ishu na kutegemewa itapata rungu zito kutoka FA. Lakini FA imesema haitoiadhibu klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment