Friday, 12 May 2017

Sanchez anatamani atue Chelsea hata leo

Mchezaji nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez ambaye amekuwa akilazimisha kuondoka ndani ya klabu yake ya sasa ya washika bunduki wa London ni kama anatamani usajili wake wa kuja Chelsea ufanyike haraka na azivae 'jersey' za The Blues mara baada ya kutuma 'post' katika mtandao wa Instagram akionyesha kama kutaka kuondoka klabuni hapo na hana mpango wa kuendelea kubaki katika klabu hiyo.

Alisema "Ukitaka kujua historia yako basi tazama ulipo, ukitaka pia kujua kesho yako itakuwaje basi angalia leo unafanya nini" ambapo kwa kauli hiyo inatafsiriwa na wachambuzi wa soka kwamba kukosa kwake mataji ndani ya klabu hiyo ya Arsenal ni kwa kuwa alifanya makosa kutua klabuni hapo na haendelei kuamini kama klabu hiyo itamtengenezea mustakabali mzuri wa maisha yake ya kesho.

Ikumbukwe pia baada ya Arsenal kutolewa katika mashindano ya klabu bingwa ya Ulaya msimu huu dhidi ya Bayern Munich jumla ya magoli 10-2. Mchezaji huyo alilalamikiwa kununiana na wenzake na pia raia wa Chile ambao pia ndo nchi ambayo alizaliwa mchezaji huyo walipanga kufanya maandamano ili kumshinikiza mchezaji huyo ili kuachana na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.