Friday, 12 May 2017

Mourinho azidi kumfatafata Willian

Jose Mourinho ameendelea na nia yake ya kutaka kumsajili mchezaji nyota wa Chelsea, Willian ambaye amekuwa hana msimu mzuri chini ya Conte ambapo mpaka sasa ameanza michezo 13 tu chini ya kocha huyo huku Pedro ambaye anacheza naye nafasi moja akionekana kuaminika sana.

Willian ambaye alianza vyema na kocha huyo muitaliano lakini mambo yakaanza kuwa hovyo kwake pale tu alipofiwa na mama yake naye baada ya kurudi akakuta tayari Pedro alikuwa katika ubora wake na kusababisha Willian kuanza kusugua benchi.

Willian ambaye alikuwa chini ya Mourinho kwa misimu zaidi ya miwili akiwa nyota mkubwa katika kikosi cha Chelsea pindi ilipokuwa chini ya Mourinho amekuwa akihusishwa kutua katika klabu ya Man utd ambayo ipo na kocha huyo ambaye bado anataka kuendelea kuijenga klabu yake.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.