Eden Hazard ametoa kauli ambayo ni faraja haswa kwa mashabiki wa Chelsea.
Mchezaji huyo ambapo alisajiliwa akitokea Lille ambaye alisajiliwa mwaka 2012 amekuwa akihusishwa kwa ukaribu na klabu ya Real Madrid ambayo pia ilimtaka kabla ya kusajiliwa na Chelsea mwaka huo lakini aliitosa na kutua London katika klabu inayopatikana mitaa ya Fulham.
Amesema "sihitaji kwenda La Liga (Ligi ambayo Real Madrid inapatikana) ili kushinda Ballon d'or ila nitashinda tunzo hiyo nikiwa hapahapa Chelsea."
Kauli hiyo ni kama inawakata maini Real Madrid ambao wamekuwa wakimfukuzia mchezaji huyo kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment