Antonio Conte anatarajiwa kumrudisha beki wa kushoto wa Chelsea aliye kwa mkopo katika klabu ya Schalke 04, Baba Rahman ambapo alisajiliwa na Chelsea kwa dau la £14milioni.
Mchezaji huyo ambaye hakuwa na mafanikio ndani ya Chelsea aliposajiliwa na klabu hiyo yenye maskani yake London Magharibi na ndipo akapelekwa kwa mkopo katika ligi aliyotokea ya Bundesliga lakini safari hii akiwa Schalke 04. Hajafanikiwa sana kuonyesha kiwango chake ndani ya klabu hiyo ambapo alipatwa na majeraha ya goti na muda mwingi kuutumia akiwa nje amepangwa kurudishwa katika klabu hiyo ambapo Conte anataka kukiimarisha kikosi ili kuingia kwenye klabu bingwa ya Ulaya msimu ujao.
Jambo pekee kwa Baba anatakiwa awe fiti ili kuweza kuonyesha umahili wake na kuonyesha juhudi dhidi ya mchezaji mwenzake ambaye wanacheza nafasi moja ndani ya klabu hiyo ya Chelsea, Marcos Alonso ambaye naye amekuwa na msimu mzuri ndani ya Chelsea na ameendana sawa na mfumo wa Conte.
Je ataweza???
No comments:
Post a Comment