Mchezaji wa Man utd ambaye ndiye alivunja rekodi ya dunia ya kusajiliwa kwa dau kubwa duniani, Paul Pogba amekosolewa baada ya kusema kuhusu kulinganishwa kwake yeye na mchezaji nyota wa Chelsea aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu N'golo Kante pale aliposema;
"Kushindanishwa kwangu dhidi ya Kante nadhani ingekuwa sahihi kama tungekuwa tunaangaliwa kwa kufunga magoli"
Lakini mchezaji wa zamani wa Man utd ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa mpira Garry Neville amesema;
"Ni ujinga kwa Pogba kujilinganisha na Kante maana kazi zao zinatofautiana huyu anatakiwa afunge na kuchezesha timu lakini mwengine anatakiwa akabe na kuzuia mashambulizi"
N'golo Kante ambaye usiku wa jana alifanikiwa kutwaa tunzo na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu marufu kama PFA ambapo aliwabwaga mchezaji mwenzake wa Chelsea, Eden Hazard, Ibrahimovic wa Man utd, Harry Kane wa Tottenham, Romelu Lukaku wa Everton na Phillipe Coutinho wa Liverpool.
No comments:
Post a Comment