Wednesday, 10 May 2017

Conte aishawishi Chelsea ifanye haraka kwa Morata

Alvaro Morata ndilo jina la kwanza la wachezaji ambao Conte anatamani wavae jezi za Chelsea msimu ujao.

Antonio Conte ameongea na bodi ya usajili ya Chelsea kwamba ifanye inavyoweza kumleta mchezaji huyo darajani. Conte anaamini kuja kwa Morata ndani ya Chelsea akitokea Real Madrid kutaongeza kasi na nguvu kuweza kufanya vizuri msimu ujao haswa kwenye klabu bingwa ya Ulaya maarufu kama Uefa Champions League.

Antonio Conte ambaye kabla alishawai kufanya kazi na mchezaji huyo wakiwa Juventus anaamini ili kuongeza kasi ya ufungaji na Chelsea kuwa hatari basi analazimika kutengeneza kikosi bora zaidi kuliko hichi cha sasa ambapo kwanza haijacheza michezo mingi maana haikuwa na mashindano yoyote ya nje ya Uingereza.

Alvaro Morata ambaye mpaka sasa ameanza michezo 13 na kutokea benchi michezo 11 amefanikiwa kuifungia klabu yake hiyo ya Real Madrid jumla ya magoli 15 lakini bado ameonekana kutoaminika zaidi na kwa hivyo timu kadhaa zimeonyesha nia ya kumtaka Chelsea nayo ikiwa mojawapo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.