Kumekuwa na fununu nyingi juu ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambapo amekuwa akihusishwa na kutakiwa na Inter Milan ambayo ipo chini ya tajiri mpya.
Baada ya fununu zote hizo, kocha huyo mwenye uraia wa Italia amefanya mkutano na waandishi wa habari na kusema bado yupo Chelsea na ataendelea kubaki sana.
"Nipo hapa na nna mkataba bado na Chelsea, nina miaka miwili zaidi na klabu hii. Na kwa kawaida kocha au mtu anapojiunga kufanya kazi na timu fulani anatamani kuendelea na kubaki zaidi na timu hiyo" amesema kocha huyo wa Chelsea.
Kocha huyo anakaribia kuipa ubingwa klabu hiyo ya Chelsea yenye makao yake London Magharibi ambapo amebakiza mchezo mmoja ili kutawazwa rasmi kuwa bingwa wa Ligi kuu ambapo usiku wa leo inatarajiwa kushuka dimbani ugenini dhidi ya West Bromwich Albion ambapo kama ikishinda mchezo wa leo itafikisha alama 84. Ambapo kwa maana hiyo itamaanisha mpinzani wake Tottenham mwenye alama 74 hata kama akishinda michezo yake yote mitatu aliyobakiwa nayo hatoweza kuishusha Chelsea.
No comments:
Post a Comment