Chelsea imebakiza alama tatu ili kutambulishwa rasmi kuwa mabingwa wapya, hii inatokea baada ya msimu uliopita kuwa mgumu kwa klabu hiyo na kuishuhudia ikimaliza katika nafasi mbaya ambayo hakuna aliyewai kufikiri kuwa ingemaliza katika nafasi hiyo.
Lakini leo imetoka kwenye nafasi mbaya ile ya msimu uliopita mpaka kuongoza ligi na kubakiza alama 3 tu kuitwa mabingwa wa Uingereza.
Ni nani aliyeitoa chini? Ni nani alisaidia kutengeneza timu bora ambayo leo imekuwa tishio?
Bila shaka jibu ni Antonio Conte.
Ameleta muhimili mpya na kuifanya ile Chelsea iliyoshika nafasi mbaya msimu uliopita leo kuwa timu bora zaidi na mfumo wake wakiitaliano wa 3-4-3.
Sasa ligi inaelekea mwisho na Chelsea imebakiza alama 3 kuwa mabingwa huku wakiwa na michezo 3 iliyobaki.
Chelsea inatarajiwa kumuongezea mkataba mpya kocha huyo ambayo amekuwa na msimu mzuri na hapo pia Inter Milan ambayo imepata maboss wapya imetangaza kumuwania kocha huyo ikitaka huduma yake.
Nadhani Chelsea inapaswa ifanye haraka maana baada ya klabu hiyo ya Inter Milan kupotea kwenye ramani ya soka sasa inataka kurudi kwa kishindo na kwa maana hiyo wanataka kumtumia Conte awe mmoja wa watu watakayoirudisha Inter kwenye zama zile za ufalme wao.
No comments:
Post a Comment