Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameamua kusitisha mazungumzo baina yake na uongozi wa klabu ya Real Madrid juu ya usajili wa mshambuliaji Alvaro Morata.
Antonio Conte amesitisha usajili huo baada ya kuhofia huenda kama akishinikiza usajili wa mchezaji huyo mwenye uraia wa Hispania kutua Chelsea basi Real Madrid ambao ndio wanaommiliki mshambuliaji huyo watatumia njia hiyo kuomba wabadilishane mchezaji huyo na Courtois au Eden Hazard.
Thibaut Courtois amekuwa akifukuziwa na Madrid kwa muda mrefu na hata Eden Hazard pia amekuwa akitajwa kuhusishwa na usajili wa kuhamia kwa wababe hao wa Hispania ambao wamefuzu kucheza fainali ya klabu bingwa ya Ulaya. Lakini Conte bado anawahitaji sana wachezaji hao na atamani kuona hata mmoja wao akiondoka kwa hivyo ameamua kuachana na mazungumzo hayo ya kumsajili kinda huyo.
No comments:
Post a Comment