Ukisikia kubaniana na jeuri ya pesa basi ndo hii, baada ya Chelsea kumfukuzia mchezaji nyota wa Torino ambaye ndiye kibara wa mabao katika timu yake hiyo, Andrea Bellotti basi ile klabu kongwe na tishio ya zamani kutoka katika mipaka hiyohiyo ya Italia ambapo nyota huyo ndipo anapochezea, klabu ya Inter Milan imekuja tena na kusema na wao wanamtaka mchezaji huyo ambaye anatajwa kuwa na thamani ya £100milioni.
Inter Milan ambayo imepata mmiliki mpya ambaye amepanga kumwaga mahela katika klabu hiyo ili kuirudishia makali yake, imeonyesha nia ya kumtaka Bellotti ambaye pia amekuwa akifukuziwa muda mrefu na Chelsea ambayo nayo inajipanga kushiriki klabu bingwa ya Ulaya msimu ujao na kutaka kuwa na safu ya ushambuliaji yenye uimara ili kuweza kufika mbali katika mashindano hayo.
Lakini pia ikumbukwe Antonio Conte ambaye pia alionyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata ambaye kama angempata huyo basi Bellotti angeachwa lakini Conte ameamua kusimama na mpango wa kumsajili mchezaji huyo wa Madrid na kwa maana hiyo atatilia nguvu katika kumsajili kati ya Bellotti au Lukaku ampate mmoja wapo. Lakini pia wachezaji wengi nyota wanatamani kucheza klabu bingwa ya Ulaya na Inter Milan ambayo inamtaka Bellotti haina nafasi kubwa ya kushiriki mashindano hayo kwa maana hiyo Conte huenda akatumia sababu hiyo kumshawishi Bellotti atue Chelsea.
No comments:
Post a Comment